SRS ni kifupi cha kwaya ya Shekinah Revival Singers

ufuatao ni muundo wa uongozi ambao unasimamia kwaya hii

 1. 1.      Uongozi na Usimamizi wa SRS

Kutakuwa na viongozi wafuatao hapa chini na majukumu yao yatakuwa kama yalivyoelezwa chini ya kila nafasi. Viongozi hawa watakuwa madarakani kwa kipindi cha miaka miwili na baada ya hapo uchaguzi mwingine utafanyika. Viongozi watakuwa na ukomo wa uongozi wa vipindi viwili

 1.   Mwenyekiti

Mwenyekiti atakuwa na majukumu yafuatayo:-

 1. Kuongoza vikao vyote vya SRS
 2. Kuitisha vikao vya dharura kwa wakati wowote
 3. Ndiye msemaji mkuu wa kwaya (SRS)
 4. Ni mmojawapo wa watia sahihi katika akaunti
 5. Ndiye msimamizi mkuu wa shughuli SRS

Hatakuwa mwajiriwa bali atakuwa mtumishi wa kujitolea tu ndani ya SRS (kwa hiyo hakutakuwa na posho wala mshahara wa mwenyekiti)

 1. 3.      Sifa za mwenyekiti wa SRS
  1. LAZIMA awe mwanakwaya wa SRS
  2. LAZIMA awe mshirika wa kanisa la mahali kwaya ilipo
  3. LAZIMA awe na uwezo wa kuongoza kwaya
  4. LAZIMA awe mtu mwenye ushuhuda mzuri ndani na nje ya kanisa
  5. Ajue kusoma na kuandika bila matatizo
  6. Awe na maono ya kuongoza kwaya na nia
  7. Akubali kujaza fomu ya uongozi inayotolewa na SRS

 

 1. 4.       Katibu

Katibu atakuwa na majukumu yafuatayo:-

 1. Kuratibu shughuli zote za SRS chini ya mwenyekiti
 2. Kuandaa na kuitisha vikao vyote vya kamati na wanakwaya wote kama atakavyoelekezwa na mwenyekiti
 3. Atatunza muhuri na kumbukumbu zote za SRS
 4. Ni mmojawapo wa watia sahihi katika akaunti ya SRS
 5. Atawajibika kwa mwenyekiti wa umoja.
 6. Hatakuwa na posho wala mshahara labda pale ambapo wanakwaya wataona anafaa kulipwa kwa kazi zake.

 

 1. 5.      Sifa za katibu
  1.  LAZIMA awe mwanakwaya wa SRS
  2. LAZIMA ajue kusoma na kuandika vyema ili atunze kumbukumbu za kwaya
  3. LAZIMA awe msiri mkubwa wa siri za SRS Kwani neno ‘katibu’ kisawe chake katika kiingereza ni ‘secretary’  neno ‘secrete’ lina maana ya ‘siri’
  4. Awe na nia ya kutunza kumbukumbu zote za SRS

 

 1. 6.      Mhasibu

Mweka hazina atakuwa na majukumu yafuatayo:-

 1. Kutunza kumbukumbu sahihi za mapato na matumizi ya fedha za SRS
 2. Kuandaa mapendekezo ya bageti za mikutano mbalimbali
 3. Kutoa taarifa ya fedha katika vikao pindi itakapohitajika
 4. Hatakuwa mwajiriwa bali atajitolea
 5. Hataweza kutoa fedha kwa maamuzi yake binafsi bali mpaka watia sahihi wengine pia wakubali.

 

 1. 7.      Sifa za Mhasibu
  1. Awe mwanakwaya hai wa SRS
  2. Ajue kusoma na kuandika vizuri
  3. Angalau ajue hesabu za kifedha pasipo kuwa na mashaka naye
  4. Awe mwaminifu ambaye hajawahi kufuza fedha mahali popote pale

Wafuatao watakuwa washauri wakuu wa SRS pale inapotakikana

 1. Mchungaji
 2. Mwinjilisti
 3. Mashemasi
 4. Washauri pendekezwa
 5. Walezi ambao wamechaguliwa na SRS

 

 1. 2.      Mlezi wa SRS

SRS itakuwa na mlezi wa kwaya ambaye atakuwa na sifa zifuatazo:-

 1. Awe Mkristo
 2. Si lazima awe mshirika wa Shekinah
 3. Awe na uwezo wa kusaidia kuendeleza SRS
 4. Asiwe na nia ya kutumikiwa na wanakwaya
 5. Awe na moyo wa kujitoa; muda na mali
 6. Awe mdau wa injili
 7. Ataombwa kwa kuandikiwa barua na kupewa malengo ya SRS kwa mwaka
 8. Atakayeweza kushirikiana na wanakwaya na viongozi wote.
 9. Mara tu baada ya kwaya kuanza rasmi lazima mlezi apatikane ili kuweza kujua lengo la kwaya.

 

 1. 3.      Waalimu wa SRS

SRS itakuwa na waalimu wafuatao:-

 1. Mwalimu Mkuu (Kwaya masta Mkuu)
  1. Atakuwa ndiye kiongozi mkuu wa waalimu wote ambao watakuja na kukaribishwa
  2. Atahusika na shughuli zote za uimbaji
  3. Mwalimu atapaswa kupeleka nyimbo ambazo ametunga kabla ya kufundisha kwa mchungaji au mwinjilisti kwa ajili ya uthibitisho.
 2. B.     Mwalimu Msaidizi
  1. Atafanya kazi kama ambavyo ataelekezwa na kwaya masta mkuu wa SRS
  2. Atakuwa mshauri wa karibu wa kwaya masta mkuu wa SRS
  3. Kwa kushirikiana na kwaya masta mkuu kufundisha sauti kwa wanakwaya wote
 3. C.     Fundi Mitambo
  1. Atachaguliwa fundi mitambo ambaye atakuwa na uzoefu wa kuunganisha mitambo
  2. Atawajibika kupanga zamu za utunzaji wa vyombo vya mziki
  3. Atawajibika kutoa taarifa ya vyombo; ubora na uharibifu wake wakati unapokuwa umejitokeza.

 

SEHEMU YA NANE

 

Mwenendo wa kwaya kwa ujumla

 1. 1.      Mazoezi ya Kwaya

SRS itateua siku za mazoezi kwa ajili ya uimbaji. Mambo yafuatayo  yazingatiwe:-

 1. Kuwahi katika mazoezi ni jukumu kwa kila mwanakwaya
 2. Kabla ya kuanza zoezi la kwaya lazima kufanya maombi na kukiri imani ya mitume ambayo inatuunganisha na wakristo wengine ulimwenguni
 3. Hakuna kupiga kelele katika mazoezi ya kwaya vinginevyo utatolewa nje ya eneo la kwaya na kupata adhabu
 4. Hakuna ruhusu ya kutafuna kitu chochote kwenye mazoezi
 5. Hakuna kutoka nje ya mazoezi bila kibali cha mwalimu
 6. Yeyote anayekosa mazoezi lazima aombe ruhusa kwa mwalimu au kiongozi yeyote Yule.
 7. Mazoezi ya kwaya yatafanyika katika miongoni mwa siku zifuatazo:- Jumapili jioni, Jumatano, Ijumaa na Jumamosi. Wanakwaya watachangua siku mbili miongoni mwa hizo lakini siku ya Jumatano ni ya lazima.

 

 1. 2.      Mavazi ya Wanakwaya (Waimbaji)

Mwanakwaya wa SRS atapaswa kujisitiri kama ifuatavyo:-

 1. Kuvaa sare wakati wa ibada (kama itakuwa imeelekezwa hivyo na uongozi)
 2. Kama siku hiyo siyo ya kuvaa sare, basi lazima nguo inayovaliwa iendane na utamaduni wa jamii husika.
 3. Mavazi yafuatayo hayapaswi kuvaliwa wakati wa ibada:-Suluari kwa wanawake au gauni kwa wanaume, Sketi fupi kwa wanawake, Nguo zinazoachia kwapa, Nguo zenye maneno ambayo hayafai na Nguo zenye picha katika sehemu ya mbele

 

 1. 3.      Uchaguzi wa Nyimbo za kuimba katika Ibada.
  1. Mwalimu wa kwaya atawajibika kuchagua nyimbo na kuwaomba waimbaji wapendekeze kwa kadri ipasavyo.
  2. Mwalimu anaweza kuwaruhusu wanakwaya wachague nyimbo za kuimba katika ibada
  3. Nyimbo zitakazoimbwa zinapaswa ziendane na mahubiri ya ibada husika
  4. Wanakwaya watapaswa kufanya mazoezi kwa nyimbo za tenzi au tenzi ili kuepuka mkanganyiko unaoweza kujitokeza katika ibada husika
  5. Nyimbo yoyote ile ikishachaguliwa haiwezekani kubadilishiwa ndani ya ibada kwani ni lazima nyimbo ziandaliwe.

 

 1. 4.      Nyimbo za Kurekodi

Waimbaji wapatapo nafasi kiuchumi wataruhusiwa kurekodi nyimbo zao kwa makusudi yafuatayo:-

 1. Kutunza nyimbo zao zisisahaulike
 2. Kutangaza neno la Mungu kupitia audio na video
 3. Si kwa ajili ya kutumia kanisani katika ibada

 

 1. 5.      Tabia ya Mwanakwaya wa SRS

Mwanakwaya anapaswa ajue kuwa ni yeye ni mhubiri wa injili sawasawa na watumishi wengine wanaohubiri kwa kusema. Tofauti yake ni kuwa yeye anatumika kwa kuimba. Anapaswa basi kwa ujumla awe na tabia zifuatazo:-

 1. LAZIMA aelekeze moyo wake kwa Mungu
 2. Usafi wa mwili na roho-Mwanakwaya atapaswa kuwa msafi kimwili na kiroho kwani yeye ndiye mfano wa kuigwa na watu wengine
 3. Mwanakwaya yeyote hapaswi kutuhumiwa kwa tuhuma kama vile; uasherati, uzinzi, wizi, uongo nk. Mambo hayo yanachafuata kanisa la Mungu
 4. Mwanakwaya mpya atapimwa kwa muda utakaowekwa na viongozi wa kwaya na atapaswa kuonesha mwenendo mwema ndani na nje ya kanisa.
 5. Mwanakwaya hataruhusiwa kuongea ongea ndani ya kanisa na hasa anapokuwa amesimama kuimba
 6. Mwanakwaya lazima awe na Biblia na wimbo wa Tenzi/Sifa, kwani hivyo ni silaha kwake na ni wajibu kwa mkristo
 7. Mwanakwaya awe barozi wa Kristo popote pale anapokuwa

 

SEHEMU YA TISA

Mengineyo

 1. Kila mwanakwaya atawajibika kwa namna moja au nyingine kujitahidi kuhakikisha kwamba SRS inakuwa kwaya ya MFANO katika eneo la MADALE, DAR ES SALAAM na hata TANZANIA nzima.
 2. Mwenyekiti kwa kushirikiana na viongozi wengine atatengeneza sharia ndogo ndogo kutokana na mwongozo mama ili iweze kusaidia kuthibiti nidhamu ndani ya kwaya.
 3. Jambo lolote ambalo ni kubwa kimaamzi litapaswa kupitishwa katika ofisi ya mchungaji kwa ajili ya ufafanuzi na maelekezo zaidi
 4. Barua zote za mialiko lazima zipitishwe kwenye ofisi ya mchungaji na vipate kibali kutoka kwake. Hakutakuwa na ruhusa kwa waimbaji kuondoka bila taarifa kwa mchungaji
 5. Kila mwanakwaya atapaswa kujaza fomu ya kujiunga. Pia kutakuwa na fomu za uongozi ambapo wanaohitaji kumtumikia Mungu kama viongozi watajaza
 6. Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu ndiye mlinzi wa SRS

Ukitaka kujiunga na kwaya hii. unakaribishwa sana sana sana