MAELEZO/SIFA/FOMU/VIPAUMBELE-Soma maelezo yote

Katika kuunga mkono serikali ya awamu ya tano kwa kutoa Elimu bure, kanisa la Shekinah, chini ya Shekinah Mission Center tumeanzisha utaratibu wa kutoa scholarship (msaada wa kimasomo) kwa wanafunzi wa Shule za CHEKECHEA, MSINGI  na UPILI. Kwa kuwa serikali inalipa ada, kanisa limeamua kuwasaidia watoto wenye sifa za kupata msaada huu unifomu za shule, madaftari, vitabu vya kiada na mambo mengineyo.

SIFA ZA WAOMBAJI

a) Awe anatoka katika familia isiyo na uwezo kabisa wa kumhudumia mwanafunzi

b) Awe na uthibitisho kutoka serikali za mtaa kuwa hata uwezo kabisa

c) Awe anatoka katika mitaa ya Madale (Kisauke), Kulangwa, Mbopo na maeneo yanayozunguka eneo la Madale.

d) Awe na uthibitisho kutoka shule anayosoma unaomthibitishia kwamba yeye ni mwanafunzi kweli

e) wanaosoma shule za binafsi hawatapokea msaada

 

VIPAUMBELE VYA KUPATA SCHOLARSHIP

a) Washirika wa Shekinah watapewa kipaumbele cha Kwanza

b) Watoto wanaotoka katika familia za Kiislamu watapewa watafikiriwa zaidi

c) Watoto walio yatima watafikiriwa zaidi

________________________________________________________

Kama unahitaji scholarship, basi download fomu ujaze. Kama una swali lolote kabla ya kujaza fomu hiyo, tuma ujumbe kwenye anuani ya spctanzania@gmail.com au, senishekinah@gmail.com

MUHIMU KABISA: Kama unatarajia kutuma maombi kwa njia ya email, basi itabidi ukimaliza kujaza fomu uipige picha na kuibadilisha kwenye pdf file, kisha utume. Mwisho wa kutuma maombi ni 14/12/2017 saa 6:00 usiku. Asante.

Fomu ya maombi ya scholarship. Wd

Hakikisha unatumia fomu ambayo ina nembo ya kanisa kwa ndani. Fomu ambayo haina nembo ya kanisa haitapokelewa. baada ya kudownload print jaza ijaze.