TITLE: MAKOSA MAWILI YANAYOREKEBISHIKA

TEXT: YOHANA 4:46-54

UTANGULIZI:

Mambo muhimu katika somo hili:-

Injili ya Yohana ni injili ya pekee kabisa ambayo mwandishi wake amekuwa akielezea mambo bayana hasa kwa lengo la kuwaelewesha wasomaji wake matukio ambayo yaliyafanyika kipindi takribani miaka 60 ambayo wakati anaandika ilikuwa imepita. (maana inakadiriwa injili ya Yohana iliandika mwaka 90.

Yohana anatuonesha namna ambavyo miujiza ilifanyika pale Kana ya Galilaya.  Tukilinganisha miujiza hii tunaweza kuona kwamba:-

a)     Yote ilihusisha uaminifu (kuamini kwa mtu), kwa mfano katika Arusi ya Kana, Mariam alimwamini mwanaye kwamba anaweza kusaidia upatikanaji wa divai ambayo ilikuwa imeisha. Vivyo hivyo tunaona kuwa hapa (diwani) “afsa” aliamini kwamba Yesu anaweza kushuka kwenda Kapernaum na kumponya mtoto wake.

b)     Yote ililenga watu waweze kuamini. Katika Arusi ya kana mwishoni tunaona kwamba “wanafunzi wake wakamwamini”(2:11) lakini pia katika uponyaji wa kijana wa afsa tunaona kuwa “akaamini yeye pamoja na wote wa nyumbani mwake” (mst 53)

c)     Yote ilihusisha kundi maalum la watu. Kwa mfano katika Arusi ya Kana tunaona kuwa watu wachache tu walihusika (mama Yesu, na watumishi) (2:5). Katika muujiza wa pili tunaona kwamba unahusisha watu wachache pia (yaani baba wa mtoto na watu wa nyumbani kwake)

d)     Yote inaonekana kuhesabika, kwa mfano katika ule muujiza wa Kana tunaambiwa kwamba kuwa huo ulikuwa “mwanzo wa ishara” (2:11) lakini katika muujiza wa pili kwa hapa kana tunapewa pia maelezo kuwa ni muujiza wa ngapi. Tunasoma kuwa “hiyo ni ishara ya pili aliyoifanya Yesu, alipokuwa ametoka Uyahudi kufika Galilaya”(4:54)

Lengo letu leo siyo kujifunza muujiza wa kwanza kule Galilaya bali ni muujiza wa pili ambao unahusisha huyu diwani na mtoto wake. Kupitia muujiza huu, nataka tujifunze MAKOSA MAWILI YANAYOREKEBISHIKA ambayo huyu “diwani” aliyafanya na ambayo mara kwa mara sisi tunayafanya wakati tunapohitaji msaada kutoka kwa Mungu.

Hakuna kipindi kigumu katika maisha kama kuuguliwa. Diwani huyu alikuwa ni kiongozi mkubwa katika Capernaum ambaye historia inasema kwamba alikuwa anafanya kazi kwa Herode. Pamoja na ukuu wake, lakini ilibidi apande kwenda umbali wa kilomita 20 hivi kutoka Capernaum kwenda Cana ya Galilaya (kipindi kile hapakuwa na gari bali jamaa alitembea). Tunaweza hata kusema kwamba alijishusha sana! Hakutaka kutuma watumishi wengine kumfuata Yesu bali yeye mwenyewe aliamua kwenda kwa ajili ya kurejesha uponyaji wa mtoto wake.

Lakini katika kusafiri kwake na kufika kwa Yesu Kristo tunaona kuna MAKOSA (Mistakes) mawili ambayo nimesema yanaweza Kurekebishika (kwa sababu katika fungu hili makossa hayo yalirekebishika vizuri tu). Makosa hayo kama yasiporekebishwa yanaweza kuleta athari kubwa katika maisha yetu ya imani.

Kosa la kwanza

YESU ASHUKE (AENDE CAPERNAUM) KWA AJILI YA KUMPONYA MTOTO WAKE (MST.42)

Ukisoma kwa harakaharaka huwezi kuona kosa la diwani huyu mahali hapa,lakini ukisoma kwa makini na kutafakari utaweza kugundua mambo yafuatayo:-

a)     Yesu lazima aende kule Capernaum, yaani anaamini kwamba Yesu anahitaji kufika mahali hapo na kufanya uponyaji pengine labda kwa kumgusa mtoto wake. Wakati akienda hakuamini kwamba Yesu alikuwa na uwezo wa kuponya hata akiwa mbali.

Hebu tufikiri kwa muda mfupi (Yesu alikuwa ametembea kilometa 79 mwendo wa miguu kutoka Uyahudi hadi Galilaya, ni mwendo wa siku 2 au 3 hivi kwa mtu anayetembea haraka. Sasa hivi anaambiwa aunganishe safari nyingine ya kushuka kwenda Capernaum-kilometa kama 20 hivi), huoni kwamba Yesu kama mwanadamu alikuwa amechoka pia?

 1. Aliamini kwamba muujiza utatokea tu ikiwa Yesu yupo hapo-katika historia iliaminika kwamba muujiza wowote ule unapotokea lazima anayeufanya awe karibu na eneo la tukio, na ndiyo maana huyu jamaa alimsihi Yesu ashuke kwenda kumponya mwanaye
 • Imani yake inatofautiana na “akida” aliyetaka mtumishi wake aponywe na Yesu. (Math 8:5-8. Huyu alimkataza Yesu kuingia nyumbani mwake na kudai kwamba “aseme neno tu” na mtumishi atapona! Ni ajabu sana! Ingawa Yesu alimwambia atakwenda kumwona lakini imani yake ilimfanya Yesu asiende huko.
 • Imani mwanzo inaonekana kufanana nay a Naamani aliyeambiwa na Elisha kujichovya mara 7 katika mto na akakataa kwa madai ya kwamba anataka mtumishi wa Mungu aje amshike mkono (amwekee mkono) ili apokee uponyaji wake (2 Wafal. 5). Naye Naamani baada ya kupokea uponyaji aliamwamini Mungu wa Elisha (Israel)

App: mara kwa mara nimeona watu wengi wakisema, mchungaji asipokuja nyumbani kwangu katika hali hii ninavyoumwa hivi, siwezi kwenda kanisani kwake. Yaani watu wengi makanisani wanataka mpaka mtumishi awepo eneo la tukio ndipo waamini kwamba Mungu yuko pamoja na watumishi hao.

Kosa hili tunaweza kulirekebishaje? Tunapaswa kuamini uweza wa Yesu hata kama tusipomuona kwa macho yetu eneo la tukio lakini tunahitaji kuamini tu. Yesu alimwambia Thomaso kuwa “wa heri waaminio bila kuona” kwa sababu hiyo unapaswa kuwa na imani ya kwamba neno la Mungu linayo nguvu ya kuponya mahali popote pale ulipo. Yesu Kristo hayupo katika mwili lakini kazi zake zinaonekana katika maisha ya watumishi wake na kwa nguvu zake

Lakini pia unapaswa kuamini maombi ya mtumishi wa Mungu, hata kama akiwa mbali- amini kwamba Mungu anatenda kazi. Yesu Kristo akiwa kama Mungu anayejua Yote anayeweza kufanya jambo lolote, aliweza kumponya mtoto yule ijapokuwa alikuwa mbali.

Kosa la pili

KAMA YESU ASIPOKWENDA MTOTO ATAKUFA KABISA (MST 49)

Kosa hili linajibainisha katika mst 49 ambapo tunaona kwamba huyu diwani anamuona Yesu kama anachelewa vile kwenda kufanya uponyaji kwa mtoto wake. Anamwambia Yesu “Bwana ushuke asijakufa mtoto wangu” Lakini katika hali halisi mtoto alikuwa tayari ameshaponywa na Bwana Yesu (soma mst 50 “mwanao yu hai”)! Hii ni sentensi yenye mamlaka kabisa!

 1. Aliamini kwamba Kama Yesu atachelewa, mtoto wake atakufa- kwa sababu hiyo tunaweza kuhusisha kosa la kwanza na kosa la pili kama kosa moja lakini tofauti yake ni kwamba katika mstari huu “anaangalia suala la muda wa Yesu kufika kwenye tukio” kwa sababu kama atachelewa ama kwa hakika mtoto atakufa. Alikuwa anamsisitiza Yesu kuwahi haraka kwenye tukio.

a)     Hakuja kwamba Yeye ndiye anaweza kurudisha uzima

b)     Wakati anaongea hayo inaonekana kwamba Yesu tayari alikuwa ameshamponya mtoto huyo.

Tunawezaje kurekebisha kosa la pili?

Watu wengi tunaamini kwamba kama tukichelewa kufanya mambo fulanifulani katika maisha yetu pengine tunaweza kuvuruga mpango wa Mungu maishani mwetu. Hilo jambo halipo. Huyu jamaa alirekebisha kosa lake kwa kupokea AHADI ya kwamba “NENDA” kwa sababu mtoto wake alikuwa mzima. Biblia inasema “akalisadiki lile neno aliloambiwa na Yesu” (mst50).

c)     Aliamini ambacho Yesu alisema na akapokea wakati huo huo, na ndiyo maana alipofika nyumbani akauliza muda mtoto alipopona!

d)     Mwisho akaisababisha familia yake iamini uweza na nguvu za Yesu Kristo (Pengine Herode alisikia habari hizi na kutaka kumwona Yesu)

App: hayo ni makossa ambayo nimesema yanaweza kurekebishika! Makossa haya niliyoyaweka SIYO DHAMBI lakini yanaweza kuwa DHAMBI kama yasiposahihishwa. Tunapitia vipindi vigumu katika maisha, na tunatamani tungeona hata malaika wanashuka katika miili na kututetea, lakini njia ya Mungu siyo hivyo. Njia yake ni kuona sisi:-

a)     Tunamwamini mwanaye Yesu Kristo na uweza wake wote bila mashaka

b)     Tunamtumaini Yesu peke yake na kuamini kwamba “mkono wa Mungu siyo mfupi” kwa hiyo atagusa mahitaji yetu.

c)     Tuamini kwamba tujapopitia mapito magumu,yeye anatuona, anataka kuwa karibu pamoja nasi.

Tujirekebishe makosa yetu kwa kuamini katika NGUVU ZA MUNGU popote pale alipo. Mungu hazuiliwi na jambo lolote katika kutenda muujiza wake-tatizo ni wewe ambaye unauangalia ulimwengu katika hali ya nyama na kukosa imani

 

 

 

TITLE: TWO MISTAKE WE COMMIT WHEN WE APPROACH GOD

TEXT: John 4: 46-54

INTRODUCTION:

Highlights in this study: -

John shows us how the miracle took place at Cana in Galilee. When we compare these miracles we can see that: -

a) All involved trust- for example, at the wedding of Cana, Mary had believed his son that he can help the availability of wine that was over. Similarly, we see that here (the officer) believed that Jesus could drop to Capernaum and heal his son.

b) All focused on people that they can trust. At the wedding at the end as we see that "his disciples believed in him" (2:11), but also in healing the boy officer we see that "he believed he and his whole house" (verse 53)

c) All consisted of a special group of people. For example, in the Marriage at Cana, we see that only a few people were involved (Jesus' mother, and staff) (2: 5). In the second miracle we see that it involves too few people (is the father of the child and of his own family)

d) All seems to be counted, for example, in the miracle of Cana, we are told that it was a "the first signs" (2:11), but in the second miracle we read that "it is the second sign that Jesus did, when he had come from Judea to Galilee" (4:54)

Our goal today is not to learn the first miracle of Galilee, but the second miracle which involves an officer and his son. Through this miracle, I want to learn that this; there are two mistakes which the officer made and that occasionally we do when we need help from God.

 • Let me tell you my dear brothers and sisters, there is no difficult period in life if the illness. As we read that this man was a great leader in Capernaum whose history says that he was working for Herod. Despite his greatness, he had to go up to a distance of 20 kilometers from Capernaum to Cana of Galilee (at that time there was no car-may a chariot for rich people but probably this man walked, since it took two days). We can even say that he was very condescending! He would send other employees to follow Jesus, but he himself decided to go for restoring the healing of his son.
 • But in his travels and came to Jesus Christ, we see there two Mistakes when approaching Jesus, and these mistakes are correctable, but if we don’t correct them, there they will affect our faith in Christ.

Okay, let us observe those mistakes through the passages:-

 1. First mistake

The man believed that Jesus should go CAPERNAUM for healing his son (v's. 42)

If you read quickly, you cannot see the error of this man here, but if you read carefully you will realize the following: -

a) The man believed that Jesus had to reach that place, maybe to touch his son. Hence did not believe that Jesus was able to heal even from a distance.

Let's think for a short time (Jesus had walked kilometers 79 walking distance from Judea to Galilee, is the course of 2 or 3 days, now he told connect another journey to go down to Capernaum-kilometers as 20), probably Jesus as a man was tired too? Right?

b) The man believed that a miracle will occur only if Jesus was there, so the man begged Jesus to heal his son by going to the place.

 • • Let us observe other passages in the Bible, this man’s faith varies with the "centurion" who wanted his servant to be healed by Jesus. (Matthew 8: 5-8. He forbade Jesus to enter into his house and demanded that "just say the word" and your servant shall be healed! It's wonderful!
 • • This man’s faith looks the same as of Naaman who was told by Elisha to dip 7 times in the river and refused on the grounds that he wanted a servant of God to come and touch him by his hand to receive his healing (2 Kings. 5). But we see at the end that he was advised by his servants, and he went to the Jordan River and dipped himself and healed.  And after receiving healing he believed God of Elisha (Israel)

Application: Occasionally I have seen many people saying, pastor does not come to my home, so I want to quit going to that church. That many churches want to minister to be present at the scene when the faithful that God is with those servers.

How can we correct these mistakes? We have to believe in the power of Jesus, even if we do not see him with our physical eyes in the scene, but we just need to believe, since Jesus is with us all the time.  Jesus told Thomas that "Blessed are those who believe without seeing"

 

Second mistake

 • If child Jesus ​​does not go down, the boy was going to die (verse 49)

We see this mistake in verse 49 where we see that the man sees Jesus as a late as to make healing for her child. He says to Jesus, "Lord, Come down before my child dies" But in reality the child had already healed by the Lord (see verse 50 "your son is alive")! This is a sentence with absolute authority! It has already happened!

 • Many people believe that if we delay doing something in our lives, we can probably disrupt God's plan for our life. This phenomenon does not exist. Then we see how this man corrected this mistake? How then? He received the PROMISE from Jesus! What kind of promise?  The "GO" promise! The Bible says, "He believed the word that Jesus spoke to him" (vs 50).
 • Now lastly, we see that the man believed what Jesus said and received at the same time
 • The ultimate of this miracle was believing of the whole family (Perhaps Herod heard this news and wanted to see him)

App: my dear brothers and sisters, mistakes are not sins, but they lead us to sin against the Lord God if are not corrected. How then can we correct?

 • We have to believe in Jesus Christ and all his power without doubts
 • We have to trust in Jesus alone, that "the hand of God is not the short" so he touches our needs.
 • We have to believe that even if our path through difficulties, he sees us, and he wants to be around with us.
 • Let us correct our mistake by believing in God's power wherever he is. God is not hindered to do anything

Let us pray