MISHENIYAKANISALASHEKINAHPRESBYTERIANCHURCHTANZANIA-MADALE

Kanisa la Shekinah Presbyterian Church in Tanzania ni kanisa ambalo kwa hapa Dar es salaam lilianzishwa tarehe 18/5/2008 uko Mikocheni jijini Dar es salaam. Hata hivyo kanisa hili sio geni kwa sababu liko chini ya kanisa la PRESBYTERIAN ambalo lilianza miaka mingi iliyopita kupitia Wamisionari wa Kikorea.

Kwa hapa Madale kanisa lilianza tarehe 1/8/2014 likiwa na malengo muhimu kama ambavyo Kristo amelituma.

a)      Kutoa huduma za kiroho kwa:-

 • ·         Kuhubiri neno la Mungu kwa watu wote
 • ·         Kufanya maombezi kwa watu wenye shida
 • ·         Kutoa ushauri wa aina mbalimbali kwa ajili ya kuwakuza watu
 • ·         Kuwaimarisha watu kuwa tayari kwa ajili ya kazi ya Mungu

b)      Kulea vijana chini ya Shekinah Mission Center.

 • ·         Kuwalea vijana kuwa wanafunzi halisi wa Yesu/kuwafuasa kuwa wanafunzi wa Yesu
 • ·         Kutoa fursa kwa vijana kujihusisha na hudumao
 • ·         Kufanya vijana kuwa watumishi wa Mungu
 • ·         Kutoa fursa mbalimbali kwa elimu ya kujitambua

WABEBA MAONO: Kanisa hili lina maono yanayotoka kwa KRISTO ambapo wanaotimiliza maono hayo ni Mwl Boyeon Lee na Mchungaji Daniel John Seni pamoja na watenda kazi wengine wa kanisani na washirika wote

MOTTO: Neno halisi, Injili Halisi na Uhuru Halisi (NIU)

MALENGO

Kuna malengo ya aina mbili; malengo ya muda mfupi na malengo ya muda mrefu. Malengo haya yanafafanuliwa kama ifuatavyo:

Malengo ya muda mfupi

Katika mwaka 2015-2020 kanisa limepanga kufikia malengo yafuatayo;-

 • ·         Kila mkristo aweze kukua na kulijua neno na kumwandaa kwa ajili ya ujio wa Kristo kwa mara ya pili na kuwa tayari kwenda naye.
 • ·         Kila mkristo aweze kushuhudia na kuleta angalau watu wawili
 • ·         Kanisa liweze kufungua makanisa mapya angalau mawili kwa hapa DSM na Mkoani mawili

            Malengo ya muda mrefu

 • ·         Ni kuhakikisha kanisa hili linasambaa ndani na nje ya nchi mpaka Bwana wetu Kristo atakaporudi kwa mara ya pili duniani

FORM YA MAOMBEZI

ni fomu ambayo unaweza kui download