Mar. 31, 2017

huduma ya Shekinah

Maelezo kuhusu huduma hii

Shekinah Mission Centre siyo Shekinah Presbyterian Church Tanzania lakini vina uhusiano wa karibu sana katika huduma. Kati ya huduma hizi mbili; iliyotangulia ni Shekinah Mission Centre ambayo ilianzishwa Mwaka 1998 na mbeba maono haya ni Mmisionari Boyeon Lee kutoka Korea Kusini.

Huduma hii iko jijini Dar es salaam, eneo la Madale Kisauke, ambapo hujishughulisha na kulea vijana (wenye kuanzia umri wa miaka 18 na kuendelea-ili mradi wawe katika umri wa vijana).Kozi ya kufuasa vijana haipungui chini ya miaka 4 kwa vijana waliokubali kujizatiti katika huduma na wana nia ya kutumika

Uongozi: Tunao viongozi wawili kwa ngazi ya juu na wanachama wote ni wajumbe wa Shekinah Mission Centre

a) Mkurugenzi: Mwalimu Boyeon Lee (Mwanzilishi na mbeba maono)

b) Mch. Daniel John Seni (Msaidizi)

Malengo:

1) Kuwafuasa vijana kuwa wanafunzi wa Yesu kwelikweli

2) Kuibua utumishi ndani ya vijana na kuwasomesha Calvin Theological College

3) Kuwajengea vijana uwezo wa Kujitegemea na kuwa raia watiifu kwa Mungu kwa nchi yao

4) Kuwasaidia vijana kusoma neno la Mungu katika muono ambao watu wengi hawajawahi kuupitia

5) Kuwasaidia vijana kwa masomo ya elimu dunia (mpaka wale wanaokidhi vigezo

Sifa za kujiunga na Shekinah

1) Lazima uwe umempokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako

2. Lazima uwe na nia ya kujifunza

3) Lazima uwe na wito wa kutumika kwa namna yoyote ili na wito huo uwe mwito endelevu; siyo mwito wa msisimko

4) Lazima uthibitishwe na mchungaji wa kanisa unalosali

5) Lazima ukubali kanuni na taratibu za SMC

6) Lazima uwe utimize kipimo cha uvumilivu ndani ya SMC

7) Wakati wa kujiunga, asiwe na familia (yaani awe single) lakini baada ya kumaliza kozi anaweza kuoa au kuolewa

mengineyo: Yeyote mwenye nia ya kuanzisha kanisa popote pale hapa nchini kwetu, ndoto zako bado hazijazima, karibu sana sana. Shekinah imesajiriwa chini ya kanisa la Shekinah Presbyterian Church in Tanzania.

Kama una swali lolote; uliza hapa chini kwenye sehemu ya (Comment); viongozi watakujibu kulingana na jinsi ulivyouliza.
Karibu sana.