TAFADHALI naomba Maoni Yako

Msaada: Ndugu niko katika kazi ya uandishi wa kitabu: Ninaomba unisaidie kujibu maswali haya
1. Ili mtu aonekane amefanikiwa, na vitu gani anahitaji kuwa navyo?
2. Je ni mpango wa Mungu kufanikiwa au kuwa masikini?
3. Je kanisa linawezaje kusawasisha (harmonize) tofauti ya walio nacho na wasio nacho?
Note: a) mawazo yote yakiwa yamechambuliwa yataingizwa kwenye kitabu ikiwa tu watatoa taarifa na majina yao sahihi.
b) Wale watakaotoa maoni kupitia ukurasa huu, wataweza kununua kitabu hicho kwa nusu ya bei.
kumbuka tena: Huu ni utafiti! Napenda kujua mawazo ya wapendwa ili kuweza kuleta usawa wa hoja.
Asanteni sana.
ukipenda tumia email: senishekinah@gmail.com nami nitayapakua maoni yako.
Mch. Daniel John Seni (Shekinah Presbyterian Church)

ILI KUTOA MAONI: Tazama hapo juu utaona sehemu imeandikwa " add message, Click here!" Bonyeza hapo na andika toa maoni. KAMA UTAPENDA, UNAWEZA KUWEKA NA PICHA YAKO.

Jul. 9, 2017

Eduard Elias Bahingayi

Nianaze na andiko kutoka 3Yohana 1:2

"Mpenzi naomba UFANIKIWE katika mambo YOTE na kuwa na afya njema kama ROHO yako ifanikiwavyo"

Katika maandiko niliyoanza nayo kuna maneno matatu nimeyaandika kwa herufu kubwa ambayo ndiyo yanayojenga hoja yangu.

1. Mtu kuonekana amefanikiwa ni vile namna roho yake ilivyofanikiwa na siyo kuwa na vitu vingi au mali nyingi kuwa ndiyo kiwango cha mafakio. Kwa hiyo mtu kuwa na amani, furaha, kuridhika n.k vitu vinavyofanya roho yako kuwa vizuri. Unaweza kuwa na mali lakini
ukakosa mafanikio ya moyo kwamaana ya kuwa nahuzuni, afya mbovu, kukosa kuridhika (japo unamali)n.k hiyo inakufanya kukosa sifa ya kufanikiwa.

2. Kutokana na utangulizi wangu si mpango wa Mungu uwe masikini wala si mpango wa Mungu uwe tajiri. Mpango wa Mungu ni wewe ufanikiwe tena kama roho yako ifanikiwavyo. Kwa jinsi hiyo itategemea nini maana ya Umasikini au Utajiri ambayo inawza kufungua mjadala
mrefu. (Mhubiri 1:14) Kama maana ya utajiri ni kuwa na magari, majumba ya kifahari, na vito vya thamani harafu huku umasikini ukawa kinyume chake bila kijali ni kwa kiwango gani mtu huyo (masikini /tajiri) roho yake imefanikiwa (rejea juu ) basi huo hauwezi
kuwa mpango wa Mungu. Mpango wa Mungu ni kufanikiwa kama roho yako inavyofanikiwa.

3. Katika maana nilizotangulia kutoa hapo juu. Ndiyo kanisa linaweza kusaidia kumfanya mtu kuelewa kusudi la Mungu na hivyo kusaidia katika kufikia "mafanikio yake". Nimetumia mafaniko ya ko kwa kuwa mafaniko ya roho yako. Asnte.

Jul. 7, 2017

Patricia Geni.1.Kwa mtazamo wangu Ili mtu aonekane amefanikiwa Amani na furaha ya moyo ndivyo vinatakiwa vitawale maisha yake...pamoja na kwamba kwa mtazamo wa nje watu watapenda kuona mali ili kupata tafsiri kamili ya kufanikiwa ila mali hizo zikiwepo bila kuwa na

amani wala Furaha ndani ya maisha ya mtu bado tafsiri ya kufanikiwa inakuwa haijakamilika.Mali tuwe nazo kama ishara ya mafanikio ila AMANI NA FURAHA viambatane navyo.2.Mpango wa Mungu kwa wanadamu ni kufanikiwa.Ila mafanikio hayo yaende sambamba na kusudi la Mungu.3.Kwa mtazamo wangu ni kazi kusawazisha tofauti ya walionacho na wasionacho ktk kanisa na jamii kwa ujumla.Ila kuna njia zikitumika vizuri basi zinaweza kupunguza tofauti kubwa ya walionacho na wasionacho...Mfano ..kutoa semina za ujasiliamali ndani ya kanisa...Jinsi

ya kuweka akiba hata kwa kile kidogo unachopata pia kuwa na nidhamu ya Pesa.

Jul. 7, 2017

Patrisha

1.Kwa mtazamo wangu Ili mtu aonekane amefanikiwa Amani na furaha ya moyo ndivyo vinatakiwa vitawale maisha yake...pamoja na kwamba kwa mtazamo wa nje watu watapenda kuona mali ili kupata tafsiri kamili ya kufanikiwa ila mali hizo zikiwepo bila kuwa na
amani wala Furaha ndani ya maisha ya mtu bado tafsiri ya kufanikiwa inakuwa haijakamilika.Mali tuwe nazo kama ishara ya mafanikio ila AMANI NA FURAHA viambatane navyo.2.Mpango wa Mungu kwa wanadamu ni kufanikiwa.Ila mafanikio hayo yaende sambamba na kusudi la Mungu.3.Kwa mtazamo wangu ni kazi kusawazisha tofauti ya walionacho na wasionacho ktk kanisa na jamii kwa ujumla.Ila kuna njia zikitumika vizuri basi zinaweza kupunguza tofauti kubwa ya walionacho na wasionacho...Mfano ..kutoa semina za ujasiliamali ndani ya kanisa...Jinsi
ya kuweka akiba hata kwa kile kidogo unachopata pia kuwa na nidhamu ya Pesa.

Jul. 6, 2017

Remy

1. Kwangu mimi mafanikio ni furaha na uwepo wa amani ya ndani... vitu kama magari nyumba mashamba n.k.. ni muonekano wa nje ambao wakati mwingine hauakisi ukweli wa mafanikio.. walau kwa kuwa vingi vimepatikana kwa mikopo ambayo bado inalipwa au kwa njia
ambazo si za kawaida kama ushirikina... inatiwesha upendo ma amani kwa wahusika..2. Mpango wa Mungu ni kila mja wake awe na kiasi cha kumuwezesha kutii na kuishi katika mpango Wake... kama kufanikiwa kunakutenga na Mungu basi kwako huo si mpango wa Mungu.3. Makanisa ya sasa mengi ni ya mfumo wa una nini... tumeona makaniaa ya yanakosa "rationale" na kwa hali ya kawaida inakuwa ngumu kanisa kuhubiri habari za Lazaro.... kwa kuwa nayo yapo katika mbio za kujiimarisha kiuchumi.. so hadithi itakuwa ni ya kuwaimarisha
waumini wake... nadhani mpango mzuri ni kuwahikiza waumini kufanya bidii kayika masomo, kufanya kazi kwa bidii na kutoa elimu za matumizi mazuri ya pesa bila ya kuathiri makisanyo ya majitoleo..