CHURCH PHILOSOPHY OF THE SHEKINAH PRESBYERIAN CHURCH

Jesus Mission-our mission

3P-WFG

Daniel John Seni

________

Pure Word

Pure Freedom

Pure Gospel

We center our ministry philosophy on Mathew 9:35 “And Jesus went throughout all the cities and villages, TEACHING in their synagogues and PROCLAIMING the gospel of the kingdom and HEALING every disease and every affliction.”

 

3P-WFG

Pure Word- as Jesus was teaching the Word of God; we focus on teaching the people God’s word. To fulfill this, we develop our church education to all departments. To fulfill this we do the following:-

 • One primary strategy for making disciples is to utilize decentralized small groups and one-on-one relationships.
 • The leadership evaluates every activity by its effectiveness in producing disciples, and will modify or discontinue activities that are ineffective or that distract us from that goal
 • We offer small groups and other ministries and multiple commitment levels to develop sequential growth for disciples.
 • Bible Group study is the basic for our church education; we divide classes as follows; children, youth and adult. We teach in different groups.
 • Our adult Sunday school classes is the key integration point for the church as well as a place for fellowship and teaching
 • We establish prayer partners with each one in our church.
 • We motivate the church members to continue in their faith and knowing Jesus through his Word.

Pure Freedom-as Jesus was Healing, we also want to heal people through the Word of God. To fulfill this we establish pastoral counseling center and deliverance prayer for the demonized people.

 • We do pastoral counseling every Thursday (the whole day)
 •  We collaborate with nearby hospitals to make sure that those who suffer from different kind of disease may see the doctors. (We have a plan to establish our own clinic)
 • We create continual prayer meeting for the people to make sure that they are free from every kind of disease.

Pure Gospel-as Jesus was preaching the pure Gospel, we also preach the gospel to all people. Then here we launch evangelism team to reach the unreached group.

 • We invite the non-believers to the kingdom of God and to live a life (to imitate Jesus Christ) worthy of being called.
 • We educate brothers and sisters who are already in church, so that they may be good witnesses for the new comers.
 • We do the so called “open worship” which center on Christ and exalt God, the non-believers can join easily in our church
 • our aim is not on external appearance (goods of numbers), but rather the internal (inner being)
 • to fulfill this we have decided to divide the church (local church limit number is 100 members, and then if they exceed, we open a new branch)

Jesus Mission-Our Mission

___________________________________________________________

 

MAELEZO ZAIDI KUHUSU SHEKINAH PRESBYTERIAN CHURCH MADALE

HISTORIA FUPI

Kanisa la Shekinah Presbyterian Church ni miongoni mwa makanisa ya Kipresbyteriani hapa Tanzania. Kwa hapa Dar es salaam lilianzishwa tarehe 18/5/2008 huko Mikocheni na kuhamishiwa Madale tarehe 1/8/ 2010 na huu ukawa mwanzo rasmi wa Shekinah Presbyterian hapa Madale.

Kanisa hili linao uhusiano wa moja kwa moja na KOREA CHURCH MISSION kupitia mmisionari Wetu Mwalimu Boyeon Lee ambaye siku ya leo atatulisha neno la Mungu katika Maadhimisho haya.

Kanisa hili tangu kuanza kwake limekuwa likiongozwa na Mch. Daniel John Seni. Viongozi wengine waliopo sasa ni:-

Mashemasi:-

 1. Ernest Shimbi
 2. Elizabeth Lwagi
 3. Fabian Lukele

Wainjilisti:-

 1. Mwinj. Marko Shija—ni mwinjilist Kiongozi
 2. Mwinj. Shadrack Zakayo-Uinjilist na Umishen
 3. Mwinj. Buyeye Subidi-kwaya na mziki
 4. mwinj. Rebecca Shabaan-bado mwanafunzi wa CTC, lakini yuko chini ya Shekinah Mission Centre na hivyo kanisa linamtambua

Idara:-

Kuna idara nyingi ndani ya kanisa la Shekinah! wafuatao ni viongozi mahususi katika idara mbalimbali

1. Eliya John-ni katibu wa kanisa

2. Samsoni Nzwala-ni kiongozi mkuu wa kanda zote (kanisa tunazo kanda 3)

3. Maria Masanja-ni kiongozi wa idara ya watoto kanisani.

Kanisa hili tangu kuanzishwa kwake linajishughulisha na kuwahudumia watu KIMWILI na KIROHO pia na ndiyo maana kauli mbiu yetu ni; Neno halisi, Injili Halisi na Uhuru Halisi (NIU) kwa maana ya kwamba; kipaumbele chetu cha kwanza ni kuhakikisha tunafundisha Neno halisi na ili tuweze kufundisha neno halisi tunahitaji kuhubiri Injili halisi kwa watu wote ili waokoke na wakiokoka, na hiyo Injili halisi sasa itawaweka huru kwa Jina la Yesu Kristo!

MAFANIKIO

1)    Kanisa limefanikiwa kufundisha neno la Mungu sawasawa na mahitaji ya kanisa kupitia vipindi mbalimbali ambavyo vimeambatanishwa katika kipeperushi cha matangazo. ukiangalia kwenye matangazo katika ukurasa huu utakiona

2)    Kanisa limeweza kusaidia vijana kwa kufundisha mafundisho ya Ujasiriamali kupitia semina mbalimbali ambazo zimeendeshwa kanisani hapa kwa vipindi tofauti tofauti. Mch. Sendeu amewahi kutoa semina ya ujasiria maarifa ambayo ilikuwa na matunda makubwa.

3)    Kanisa hili ili kwenda pamoja na jamii limeanzisha masomo ya sekondari ya Elimu ya Watu Wazima kwa ajili ya kuinua kiwango cha Elimu.

4)    Kanisa limeanzisha mafunzo ya Kompyuta kwa watu wote wanaohitaji kujifunza. Tunaamini kwamba maendeleo ya Kiroho huenda sambamba na maendeleo ya Kimwili pia. Hatubagui mtu yeyote anapata mafunzo hayo

5)    Kanisa liko katika mchakato wa kuanzisha huduma Igunga-Tabora kwa hivi karibuni ikiwa ni mojawapo ya malengo yake mpaka sasa kimeshanunuliwa kwa ajili ya kanisa hilo.

6)    Kanisa kwa kushirikiana na huduma ya Shekinah Mission Centre imeweza kutuma wainjilisti kusoma katika chuo cha Calvin Theological College kilichopo jijini Dar es salaam. Chuo hiki hufundisha masomo kwa Watumishi wa Mungu kwa muda wa miaka minne.

7)    Kanisa limefanikiwa kuchapisha machapisho mbalimbali kupitia watumishi wa Mungu ambao wanao ufahamu wa hali ya juu zaidi. a) Machapisho ambayo yamechapishwa hapa ni pamoja na; Shekinah press Newsletter ambalo lina kichwa cha ‘Kila Mtu na Mvuto Wake’ b) Uwezekano wa Mkristo Kupagawa Pepo c) Tambua Uzushi d) Fungua Sasa Ukurasa wa Ajira Mbichi e) Niamue Lipi? machapisho haya yote yanapatikana kanisani Shekinah!!

8)    Mojawapo ya mafanikio mengine, ni kuwa Wanashekinah kwa msaada wa Mungu wamefanikiwa kuweka vigae jengo la kanisa kwa ndani. kwa hiyo kanisa linapendeza sana

9)  kanisa hili limekuwa kitovu cha kufundisha Wainjilisti wa kujitolea kwenda nyumba kwa nyumba. Hivi karibuni tulifanya semina ya Church mobilization ambayo ilikuwa na matunda makubwa sana

10. Kwaya ya Shekinah (Shekinah Revival Singers) imeweza kurekodi albam ya audio. hivi karibuni inajiandaa kwa ajili ya kurekodi video. kwaya iko tayari kwa mialiko mbalimbali.

UHUSIANO

Kanisa hili lina uhusiano na majirani kama ifuatavyo:-

UHUSIANO NA MAKANISA JIRANI

Kanisa hili lina uhusiano wa karibu na makanisa jirani. Ukweli huu uko wazi hasa tunapoangalia kanisa hili ni mwanachama wa UPU (Ushuhuda Pastor’s Union)- huu ni umoja wa wachungaji walio na huduma katika maeneo haya chini ya Mwenyekiti wake Mch. Daniel Ikongo. Vile vile uwepo wa wachungaji katika shughuli hii siyo jambo dogo bali inathihirisha uhusiano wetu kuwa ni mzuri. Na ndiyo maana pia leo kuna kwaya mbalimbali ambazo zimeshiriki tukio hili la kihistoria.

UHUSIANO NA TAASISI ZINGINE

Kanisa hili lina uhusiano wa karibu sana na taasisi za Elimu kwani tunaamini kwamba Elimu inao uwezo wa kubadilisha maisha ya watu. Baadhi ya taasisi hizo ni:-

 1. Atlas School. Shule hii ni jirani na kanisa hili, kwa namna moja au nyingine wamekuwa msaada wa karibu mno kwa kanisa hili na hivyo tunatambua mchango wao wa karibu katika kanisa hili. Shule hii kupitia mkurugenzi wake imekuwa ikishiriki shughuli mbalimbali za kanisa hili na imekuwa ni sehemu ya kanisa hili. Na ndiyo maana siku hizi ukiuliza kanisa huko mitaani wanasema ‘Kanisa la Atlas’ kauli hii si tu kwa sababu shule ipo karibu na kanisa hili bali ni ule uhusiano wetu. Vile vile wanashirika wa shekinah wengi wamepata ajira katika shule hii na hivyo kuwasaidia kupata fedha za kujikimu katika maisha yao.
 2. Patrick Mission High School. Shule hii iko eneo la Mivumoni. Kupitia mkuu wa shule wananafunzi wanaotoka katika kanisa hili na makanisa jirani wanapunguziwa ada (labda pengine mkuu wa shule anaweza kusema leo ada ambayo wanafunzi wanatoa)
 3.  Focus Academic Excellence (FAE) Shule hii inafundisha watoto shule ya awali (chekechekea) kupitia mkurugenzi wake imekuwa ikifundisha watoto wetu (kanisa hili bado halijawa na shule ya awali) na hivyo watoto wanafundishwa masomo ya kidunia lakini pia elimu juu ya neno la Mungu inatolewa.

UHUSIANO NA SERIKALI

 1. Kanisa pia lina uhusiano mzuri na serikali ya mtaa wa Madale. Tunashirikiana nao katika kuhakikisha tunazalisha kizazi kinachomtii Mungu. vile vile kanisa kwa kupitia waumini wote; limeamua kutoa msaada wa nguo kwa wasiojiweza. tunaandaa hafla maalumu kwa ajili ya kuwakabidhi nguo zao.

MALENGO YA  MIAKA MITANO IJAYO NI:-

Kila idara ndani ya kanisa hili ina malengo yake. Haya ni malengo ya ujumla ambayo haijalishi kwamba katika idara fulani yamewekwa.

 1. Kanisa kukua kiroho na kiidadi kutoka 80 wa sasa na kuwa waumini 150. Malengo haya yanaweza kutimia kupitia uinjilisti ambao utafanywa mara kwa mara.
 2. Kila muumini angalau alete watu wawili kwa YESU kwa miaka mitano ijayo-tunajua kwamba suala la kuhubiri Injili siyo la wachungaji na wainjilisti bali wakristo wote wanapaswa washiriki kwa asilimia mia moja kabisa!
 3. Kanisa litapanda angalau makanisa mawili nje ya Dar es salaam na hata ndani ya jiji hili-kazi hii itawezekana kulingana na juhudi ya kupeleka watumishi wetu katika chuo chetu cha Calvin Theological College.
 4. Kila mkristo aweze kumiliki uchumi wake. Kanisa litafundisha vijana na watu wengine ili kuweza kujitambua na kuweza kujikwamua katika masuala mbalimbali kupitia wadau wake.
 5. kanisa kuendelea kusaidia jamii ya watu walio katika hali ngumu ya maisha; wajane na yatima ambao hawana watu wa kuwasaidia.
 6. Kanisa litaendelea kufundisha Neno halisi, kuhubiri Injili halisi na kuwapatia watu Uhuru halisi kupitia jina la Yesu Kristo. Na hivyo kanisa litakuwa limewaandaa waumini kwa ujio wa Yesu kwa mara ya pili.
 7. kanisa kuandaa semina angalau kila mwaka semina 3 za masomo mbalimbali

katika mambo yote, tunaomba maombi yako zaidi na zaidi

Mch. Daniel John Seni

(Mchungaji Kiongozi)

kwa ajili ya ushauri na maswali; jaza ukurasa ulio hapo chini